Hizi Ndiyo Faida Kumi (10) Za Kula Ukwaju!
Unatakiwa ujaribu kuweka ukwaju karibu katika kila mlo wako kwa kila
siku kwasababu ukwaju una faida nyingi kiafya ambazo hakika zitakufanya
uwe na afya njema au kukuimarisha afya yako kiujumla
Watu waishio bara la Asia, Carribian na America ya kusini wanajua kuwa kula ukwaju maana yake ni Afya Njema.
Ukwaju unaoliwaa katika maeneo haya maeneo hayo una faida nyingi kwa watu wanaoula.
Vifundo hivi ndiyo ambavyo watu wanakula ili kupata virutubisho na faida za kiafya za ukwaju.
Ukwaju una ladha faluni ya uchachu ukiwa bado mchanga, lakini kadiri unavyozidi kukomaa unakuwa na ladha tamu. Ingawa ukwaju unakuwa na utamu kadiri unavyokuwa na kukomaa, kiujumla ukwaju ni mchachu.
Katika nchi kama Jamaica, Mexico, Aruba na India, ukwaju unachanganjwa na sukari na kuuzwa kama pipi katika mitaa na madukani. Kula ukwajua au bidhaa zitokanazo na ukwaju kuna faida sana. Ukwaju umejaa Vitamini, fiber, potassium, magnesium na virutubisho vingine muhimu kwa afya njema.
Lakini kati ya faida zingine nyingi za virutubisho na kiafya za ukwaju, kuna kadhaa ambazo ni za muhimu zaidi, na ni kama zifuatazo:
1. Ukwaju chanzo kizuri sana cha antioxidants ambazo zinasaidia kupigana na saratani. Ukwaju una carotenes, Vitamini C, flavanoids na vitamin B zote.
2. Ukwaju unakuepeusha na ukosefu wa Vitamini C.
3. Ukwaju unasaidia kupunguza homa na kukupa ulinzi dhidi ya mafua.
4. Ukwaju unakusaidia kuyeyusha chakula tumboni.
5. Ukwaju unakusaidia kutibu matatizo ya nyongo.
6. Juisi ya ukwaju hutumika kama kitu cha kustarehesha mwili.
7. Ukwaju unapunguza cholesterol mwilini.
8. Ukwaju unasaidia kuwa na moyo wenye afya njema.
9. Ukwaju ukiunywa unasaidia kupooza koo.
10. Ukwaju ukiupaka kwenye ngozi unasaidia kutibu uvimbe Kwa Tanzania ukwaju unapatikana kwenye masoko karibu yote.
0 comments:
Post a Comment