Chipukizi wa Tanzania apiga dakika tisini, Mabingwa Kenya wakishinda
Kocha wa zamani wa Azam, George Nsimbe ambaye kwa sasa
anawafundisha mabingwa wa Ligi Kuu Kenya, Tusker alimchezesha kiungo wa
Tanzania Abdul Hillary Hassan kwa dakika zote 90 dhidi ya Palos.
Katika pambano hilo la kirafiki lililopigwa jijini Kisumu, Kenya Tusker waliibuka na ushindi wa mabao 4-2.
Tusker walianza kufunga bao LA kuongoza dakika ya 34 kupitia kwa Noah Wafula aliyeunganisha kwa kichwa krosi ya Samuel Olwande.
Tusker walipata bao la pili kupitia kwa Michael Khamati dakika ya
40 lakini Eustus Ochieng’ akawafungia wenyeji Palos bao dakika moja
baadaye na kuwafanya Tusker kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-1.
Kipindi cha pili mghana Stephen Owusu aliipatia Tusker bao la tatu kabla ya Victor Ndinya kuongeza la nne.
John Wanda aliifungia Palos bao la pili la kufutia machozi na kuufanya mchezo kumalizika kwa ushindi wa Tusker wa mabao 4-2.
Abdul alisajiliwa hivi karibuni na mabingwa hao wa Kenya
wanaojiandaa kucheza dhidi ya Al Hilal ya Sudan katika Ligi ya Mabingwa
Afrika.
0 comments:
Post a Comment