Mtanzania atua Ukraine kwa Shevchenko
Wigo wa wachezaji wa Tanzania kucheza soka la kulipwa nje ya nchi unazidi kuongezeka, kwani orodha ya vijana wanaopambana kwenda kucheza nje inaongezeka na hasa katika bara la Ulaya.Kiungo wa zamani wa timu za vijana Serengeti Boys na Ngorongoro Heroes, Hamis Mroki (Haminho) aliyekua akicheza soka la kulipwa nchini Thailand (Kabin United) amepata dili ya kujiunga na klabu ya FK U’nhulets Petrove inayoshirki ligi daraja la kwanza nchini humo.
Baada ya mkataba wake kumalizika na klabu yake ya zamani Thailand, Mroki anatarajiwa kuonekana katika uzi wenye rangi ya bluu na njano msimu ujao kwenye klanbu ya FK U’nhulets Pertove.
Mroki aliyekulia katika kituo cha TSA kilichokuwa chini ya TFF na kuzichezea timu za vijana Serengeti Boys, Ngorongoro Heroes anakwenda kuungana na mchezaji mwingine mtanzania waliyekua pamoja katika timu za vijana Alfredy Amede.
Ukraine ni nyumbani kwa mshambuliaji wa zamani Dynamo Kyiv, AC Milan na Chelsea Andry Shevchenko ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa nchini humo, Ligi yake ni miongoni mwa ligi zinatoa upinzani mkali ngazi ya vilabu barani ulaya kupitia vilabu vyake vya Dynamo Kyiv, Shaktar Donetsk, Dnipro nk.
Ukiachilia mbali Mbwana Samatta anayecheza Ligi Kuu ya Ubeligiji, Thomas Ulimwengu aliyepo AFK Eskiltuna ya Sweden, Adi Yusuph Grimsby Uingereza, Alfrey Amede (Ukraine), Emily Mgeta (Uujerumani) na sasa kiungo Hamis Mroki pia anakwenda kuanza maisha mapya nchini Ukraine.
0 comments:
Post a Comment