BOFYA HAPA KUPAKUA AU KUDOWNLOAD FORM
Mfano wa form hiyo apo utakayo ipakua ni hii apa chini
Kumbuka download form isikopy mfano
FOMU YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2018/2019
HALMASHAURI YA (W) BUSOKELO SHULE YA SEKONDARI LUFILYO S.L.P 362
TUKUYU.
SIMU Na. 0756025516/0755979716
Mzazi/ Mlezi wa mwanafunzi .....................................................................................
S.L.P.............................................................
YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI LUFILYO KIDATO CHA TANO JULAI 2018.
Nafurahi kukuarifu kuwa umechaguliwa kujiunga kidato cha tano katika shule ya sekondari Lufilyo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 shule ipo katika
Halmashauri (W) Busokelo –
Tukuyu mkoa wa Mbeya. Ukifika Mbeya mjini panda gari za Tukuyu stand ya NANENANE (MBEYA-TUKUYU nauli Tshs 3000/=)
na ufikapo Tukuyu mjini usafiri wa Lufilyo unapatikana jirani na kituo cha mabasi kituo kiitwacho UWANJANI kwa nauli Tshs 5000/= usafiri unapatikana kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 12 jioni.
Muhula wa kwanza wa masomo 2018/2019 utaanza tarehe 09/07/2018
1.0 MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA
1.1 SARE YA SHULE NA MAVAZI MENGINE 1.1.1 WAVULANA
a) Sare ya shule ni suruali mbili au zaidi za rangi nyeusi marinda mawili na zisibane (sio vimodo) pamoja na koti lake la suti nyeusi sawa na kitambaa cha suruali shati mbili au zaidi nyeupe za mikono mirefu pamoja na tai
ndefu nyeusi. Jozi mbili za viatu vya ngozi rangi nyeusi vya kufunga na kamba visivyo na mchongoko na jozi mbili za soksi nyeusi ndefu zisizo na maandishi wala picha pamoja na mkanda. Kwa wanaosoma sayansi aje
na koti jeupe kwaajiri ya mazoezi ya vitendo wakiwa maabara. (Laboratory coat.)
b) Shuka mbili rangi ya bluu, blanketi, chandarua, mwamvuli, tochi kwa tahadhari na godoro la futi mbili na nusu kwa sita. T. shirt moja au zaidi za kora rangi ya dark bluu
na ufito mweupe kwenye kora na mikononi za kuvaa baada ya masomo zitakazopatikana shuleni (kwa Tsh 10000/=) pia fulana moja na bukta
zisizo na maandishi wala picha, raba jozi moja kwa ajili ya michezo na track-suit nyeusi yenye ufito mweupe mikononi
na miguuni.
MAHITAJI YA BWENINI – aje na ndoo mbili, fagio chelewa, hard broom, mopa, jembe lenye mpini pamoja na fyekeo. Pia sahani, kikombe, bakuli pamoja na kijiko kwa ajili ya chakula pamoja na sanduku, (tranka).
c) Rimu moja ya karatasi A4 ni Lazima iletwe.
1.1.2 WASICHANA
a. Sare ya shule ni sketi mbili nyeusi zenye marinda kati yanane hadi kumi na mbili zenye urefu unaogusa viatu na koti lake la suti la rangi nyeusi sawa na kitambaa cha sketi, shati mbili rangi Right Blue za mikono mirefu pamoja na tai nyeusi. JOzi
mbili za viatu vya ngozi rangi nyeusi vya kufunga na kamba visivyo na visigino virefu na jozi
mbili za soksi nyeupe ndefu zisizo na maandishi wala picha. Nywele fupi na kwa waisilamu aje na hijabu ya rangi ya Right Blue sawa na rangi ya shati iliyondefu ambayo atavaa
pamoja na uniform na shamba dress. Kwa wanaosoma sayansi aje na koti jeupe kwa ajiri ya mazoezi ya vitendo wakiwa maabara. Laboratory coat.
b). Shuka mbili rangi ya pinki, blanketi, chandarua, mwamvuli, tochi kwa tahadhari na godoro la futi mbili na nusu kwa sita.
c). Shamba dress mbili rangi ya zambarau lenye mshono wa solo lenye laining. Taulo moja na na kitenge kimoja tu. T. shirt moja au zaidi za kora (form six) rangi ya dark bluu na ufito mweupe kwenye kora na mikononi za kuvaa baada ya masomo zitapatikana shuleni (kwa Tsh 10000/=)
pia fulana moja na bukta zisizo na maandishi wala picha, raba jozi moja kwa ajili ya michezo na track- suit nyeusi yenye ufito mweupe mikononi na
miguuni.
MAHITAJI YA BWENINI – aje na ndoo mbili, fagio chelewa, hard broom, mopa, jembe lenye mpini pamoja na fyekeo. Pia sahani, kikombe, bakuli pamoja na kijiko kwa ajili ya chakula pamoja na sanduku, (tranka).
d). Rimu moja ya karatasi A4 ni Lazima iletwe.
N.B kwa wote: ni marufuku kuja na mavazi mengine tofauti na vyaliyotajwa hapo juu (ya nyumbani). Ni marufuku kuja na simu, ukikamatwa na simu utafukuzwa
shule mara moja. Pia ni marufuku kutumia vyombo vya umeme kama pasi, hita, jiko n.k vipodozi kama wanja, ina, rangi ya kucha, poda n.k haviruhusiwi kabisa.
1.2 ADA NA MICHANGO YA SHULE
a. Ada ya shule kwa mwaka ni shilingi elfu sabini (Tshs 70,000/=) unaweza kulipa Tshs 35,000/=, katika muhula wa kwanza na wapili Tshs 35,000/= au kulipa fedha yote Tshs 70,000/= kwa mkupuo.
b. MICHANGO MINGINE NI KAMA IFUATAVYO:
Tahadhari Tsh 5,000/= kitambulisho Tshs 6,000/= nembo ya shule Tsh 2,000/= kuwalipa wapishi, walinzi na vibarua wengine Tsh 30,000/= taaluma Tshs 20,000/= matibatu Tshs 10,000/= ukarabati wa samani Tshs 15,000/= mitihani ya kujipima Tsh 20,000/=.
Ada na michango yote kwa mwaka 2018/2019 ni Tsh 178,000/= na kwa muhula ni Tsh 143,000/=.
Ada na michango mingine yote ilipwe kwenye akaunti ya shule: LUFILYO SECONDARY SCHOOL Na. 61403500097 NMB Tawi lolote lile (mahali popote). Na mwanafunzi aje na (BANK PAY INSLIP).
“KARIBU SHULE YA SEKONDARI LUFILYO”
………………………… IGNASKOMBA
MKUU WA SHULE (0756025516)
0 comments:
Post a Comment