Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA), limetangaza viwango vipya vya ubora wa soka duniani kwa mwezi Februari, 2017 huku Tanzania ikiporomoka kwa mara nyingine.
Tanzania imetupwa kwenye nafasi ya 158 ikiwa na alama
152 ikiporomoka kwa nafasi mbili kutoka mwezi uliopita ambapo ilikuwa
katika nafasi ya 156.
Barani Afrika
Kufuatia mafanikio makubwa ya kubeba taji la Kombe la
Mataifa ya Afrika Jumapili iliyopita, Camerron imepanda kwa nafasi 29
katika viwango vilivyotolewa.
Cameroon inakamata nafasi ya 33 duniani ikiwa mbele
ya Austria na nyuma ya Iran. Misri waliofungwa na Cameroon pamoja na
wenyeji Gabon wamepanda pia. Misri wamesogea hadi nafasi ya 23 huku
Gabon waliotolewa katika hatua ya makundi wakipanda kwa nafasi 21 na
kushika nafasi ya 87
Kuna mabadiliko ya timu moja tu katika orodha ya kumi
bora baada ya Ufaransa kuipiku Colombia na kutua namba 6 ilhali vinara
Argentina wakiendeleza uongozi wao wakifuatiwa kwa ukaribu na Brazil na
Ujerumani katika nafasi ya pili na ya tatu.
Ukanda wa Afrika Mashariki
Uganda imeendelea kuongoza licha ya kuporomoka kwa nafasi
mbili na kutua nadasi ya 73 duniani, wanfuatiwa na Kenya katika nafasi
ya 87.
0 comments:
Post a Comment