Kavumbagu asajiliwa Ethiopia
Baada ya mipango yake ya kucheza soka la kulipwa nchini Vietnam kukwama, mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Azam, Didier Kavumbagu amekamilisha uhamisho wa kujiunga na klabu ya EPCO ya nchini Ethiopia.
EEPCO inayomilikwa na shirika la umeme la Ethiopia na kujulikana zaidi kama Mebrat Hayl imeamua kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu baada ya kunusurika kushuka daraja msimu uliopita.
Kavumbagu aliichezea Yanga kwa misimu miwili kabla ya kujiunga Azam na kudumu kwa miaka miwili pia. Aliachana na Azam mwishoni mwa msimu uliopita na kukimbilia nchini Vietnam lakini licha ya kusaini mkataba na mojawapo ya klabu nchini humo alishindwa kukamilisha uhamisho wake.
0 comments:
Post a Comment